Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), kilianzishwa mnamo 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki.
CHAWAKAMA huandaa makongamano kwa nia ya kuwapa wanachama fursa za kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili, kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa Kiswahili na kueneza Kiswahili ndani na nje ya nchi.
Kiswahili kinapopata mashiko na kupaa kwingine tujitahidi tupae nacho. Tuwe mabalozi wakukitetea popote kwa njia yoyote.
Tuutetee utamaduni wetu kupitia Kiswahili, tuondoe mipaka kupitia Kiswahili,tukitumie Kiswahili ni rasilmali yetu.