CHAKILU
Hiki ni chama cha wanafunzi wa chuo kikuu cha Lukenya
CHAKILU
MAELEZO KUHUSU CHAKILU

Chama cha Kiswahili Lukenya (CHAKILU) ni chama cha wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Lukenya. Chama hiki kilianza mwaka wa 2022 chini ya uongozi wa Joshua Kalimbo na baadae mnamo mwaka wa 2023 bwana Samuel Kungu Gichungu akawa ndiye mwenyekiti wa chama hiki. Kupitia uongozi wake, Bwana Samuel ameweza kuwaleta si wanafunzi tu wa lugha ya Kiswahili bali ni wanafunzi wote ambao wanayoipenda lugha hii.
SABABU ZA KUWEPO KWA CHAMA HIKI
Kwa kawaida, kumekuwa na matatizo mengi katika lugha yetu pendwa ya Kiswahili. Lugha hii bali kuwa ni yetu kama Waafrika imekuwa ni lugha ambayo inafifia kila uchao. Hii ni kwa sababu, mwingiliano wa mambo ya kigeni kama vile Lughaza kigeni kwa mfano ile ya Kiingereza, utamaduni wa wageni na teknolojia, zimesababisha lugha ya Kiswahili kukabwa kwa sana bila ya kuendelea ifaavyo. Ili kutatua tatizo hili, CHAKILU ilianzishwa ili kuwaleta pamoja watu wa nyanja mbalimbali ambao wataweza kuwahamasisha wengine kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha yetu, si lugha gumu wala lugha ambayo haiwezi kueleweka kwa urahisi. Washika dau wengi(ambao ni wanafunzi hapa) wako na taajiriba na ueledi mpana katika nyanja mbalimbali kama vile uandishi wa vitabu, utunzi wa nyimbo na mashairi, na ubunifu mwingi ambao ukiletwa pamoja utaweza kufanikisha Lugha ya Kiswahili kueleweka kwa urahisi.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kawaida ila ina uzito ambao, kwa pamoja, unaweza kuwaleta jamii za Wakenya kwa pamoja, na si wao tu mbali ni Jamii ya Kiafirika pia. Lugha ya Kiswahili huwa na kumbukumbu nyingi za kihistoria ambazo, hutuonyesha kuwa sisi ni Waafirika na tunapaswa kujivunia kuwa Waafrika. Lugha ya kiswahili pia imeweza kuhifadhi utamaduni wa Waafirika na ndo maana katika tamasha za kiutamaduni katika Chuo Kikuu cha Lukenya, kazi ambazo zinatumia lugha hii hupewa kipau mbele bila ya kuibagua. Kazi hizi ni pamoja na mashairi ambayo wanachama ndo huyatunga na kuyakariri pia. Kwa mfano, katika tamasha za mwaka huu (2024) shairi ambalo lilikaliwa na wanachama hiki waliweza kuibuka nambari ya kwanza.
MUSTAKABLI WA CHAKILU
Chama cha Kiswahili Lukenya imengazia kufanikisha mambo yafuatayo:
- Kuwa miongoni mwa vyama tanzu wa CHAWAKAMA na pia kutambulika kuwepo kwa chama hiki.
- Pia kuwaleta pamoja washika dau wengi kwa pamoja ambao wataweza kukipigania na kukiendeleza Kiswahili kote duniani.
- Kuwasaidia wanafunzi wengi ambao wanavipawa vya uandishi na utunzi wa kazi mbalimbali za kifasihi kama vile nyimbo, mashairi, michezo ya kuigiza na kadhalika.
- Mwisho ni kuweza kujenga msingi mwema wa Lugha ya Kiswahili na pia kuleta kujivunia kwa watu wengi kuwa wanaienzi Lugha hii.
HITIMISHO
Nachukua fursa hii kushukuru CHAWAKAMA kwa kutupa mahala ma kufanikisha kazi zetu mbalimbali. CHAWAKAMA wamekuwa wa msaada kwetu na pia kutuweka katika hadhi ya juu zaidi.
Shukran nyote
MWANDISHI
SAMUEL KUNGU GICHUNGU.