CHAKIKE ni nini? Wengi kwa mara ya kwanza hujaribiwa kufikiri ati ni chama ama kundi la wanawake ama shirika linahusisha wanawake tu; lakini la! CHAKIKE ni akronimu ya Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu Kenyatta.
Tafsiri.
- Translate- tafsiri
- Interpret-kalimani
- Exercise- zoezi
- exercise book- daftari
- Earphone- visikizi
- Microphone- kinasa sauti
- Speaker- kipasa sauti
- Flash disk- santuri
- stairs – vidato
- Balcony- Roshni
- Wheelchair- kitimaguru

Ufupisho.
Ufupisho ni hali ya kutoa muhtasari wa matini bila kufisidi maana ya matini asilia. Vipengele vifuatavyo huzingatiwa katika kufupisha matini:
- Usomaji wa habari /taarifa lengwa kwa makini ili kuelewa.
- Udondoshaji wa mawazo makuu au habari muhimu kwa makini.
- Kuandika vidokezo vya habari kwa kutumia maneno yako mwenyewe katika nakala chafu.
- Kuunganisha hoja za habari kutumia maneno yako mwenyewe katika nakala chafu.
- Kulinganisha habari muhimu na habari ya asili.
- Kupitia ufupisho ili kuhakikisha mawazo yote muhimu yapo.
- Kuhakikisha kuna mpangilio ufaao, hoja zitiririke kwa mfuatano wa uzito.
- Kuandika nakala safi ya ufupisho.
- Kuzingatia kanuni zote za warudi katika nakala safi.
- Kuhakikisha idadi ya maneno imezingatiwa.